Friday, January 19, 2007

Wanaotumia jina la Dk. Mwiko kutapeli waonywa

Na Mwandishi Wetu
IMEBAINIKA kuwa katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi la watu matapeli wanaotumia jina la Dk.Mwiko Kuona kwa nia chafu.

Kutokana na hali hiyo, Dk. Mwiko amewataka watu hao kuiacha tabia hiyo mara moja vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kujipatia pesa kwa nia ya udanganyifu.

Akizungumza na gazeti hili Jumanne wiki hii Dk. Mwiko alisema kuwa amepata taarifa hizo na kwamba ameshawabaini watu wa aina hiyo lakini kwa ustaarabu ameamua kuwaelekeza kutoendelea tena na tabia hiyo chafu.

"Tabia kama hii si tu kwamba inaharibu jina langu bali ni kuteketeza maisha ya Watanzania wenzetu kwa sababu hawa wanaotumia jina langu hawana ujuzi na tiba asilia," alisema Dk. Mwiko.

Aliongeza kuwa anachotaka sasa ni kuwaeleza Watanzania kuwa kwa yeyote atakayejitambulisha kuwa katumwa na Dk. Mwiko hana budi kupiga simu namba 0754 602629 au 0787 602629.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwiko ameongeza kuwa anaandaa ziara kwa ajili ya kuwafikia wahitaji wa tiba ambao hawawezi kuja jijini Dar es Salaam.

"Usipofanikiwa kwenda waliko inakuwa haina maana kwani wagonjwa wengine hawamudu kusafiri kuja jijini."

Wakati huo huo, DK. Mwiko ameendelea kujenga ofisi mpya yenye uwezo wa kubeba wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.

"Watu wanaongezeka na hivyo sina budi kupanua eneo kwa kujenga ofisi mpya hapa Keko," alisema.

No comments: